Waziri Kabudi Aigaragaza Yanga Bungeni, Wanachotaka Haiwezekani Wasipocheza Derby Watakiona cha Mtema Kuni


Waziri Kabudi Aigaragaza Yanga Bungeni, Wanachotaka Haiwezekani Wasipocheza Derby Watakiona cha Mtema Kuni


Siku ya Leo jijini Dodoma kumewaka moto ikiwa ni sehemu ya vikao kwa ajili ya bajeti ya wizara ya Sanaa Michezo na Burudani. Katika Moja ya vivutio vikubwa ndani ya bunge ilikuwa la kutambulishwa kwa Fahali wawili Eng Hersi Said Na Wallace Karia.


Katika Hali ambayo iliacha Shangwe kubwa kwa wabunge ilikuwa pale ambapo Raisi wa Klabu ya Yanga alisimamishwa na Kisha wabunge kupiga meza zao huku wakisindikiza na maneno kua " Hatuchezi, Hatuchezi, Hatuchezi". Na pia baada ya kusimama Karia Hali ya kuzomea ilisikika ndani ya bunge Hilo.

Waziri Kabudi Aijibu Yanga Kiaina

Katika hatua nyingine wakati wa maswali kwenda kwa wizara husika, Mbunge Joseph Musukuma alitoka na swali kuhusu ni kwa namna gani serikali inakwenda kusemea sakata la Yanga pamoja na bodi ya ligi na TFF. Hasa kufuatia mchezo wa Derby.

Ikumbukwe kua klabu ya Yanga walituma Waraka mkubwa sio kwenda kwa TFF au bodi ya ligi, Yanga baada ya Kushindwa kesi katika mahakama ya CAS walitoka na Kuamua kuanguka kwenye miguu ya serikali kutaka haki itendeke ya kua Simba wanafanyiwa upendeleo na TFF.


Wakati wa kujibu swali Hilo Mh Palamagamba Kabudi alijibu kua Sheria za FIFA zinatoa pinzani kwa serikali ya taifa lolote mwanachama kuingilia katika mambo ya Soka ya Nchi husika. Hivyo Yanga Wanachoomba kwa serikali HAIWEZEKANI.


Kwa maana hiyo kwa sasa Yanga itabidi kuchagua ikiwa inakwenda Kucheza mchezo wake wa Derby ambayo rasmi itapigwa tarehe 15 mwezi wa 6 saa 11 jioni. Ikiwa klabu ya Yanga itagoma kushiriki mchezo huo inaweza kukutana na adhabu Kali kuliko na mbaya.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad