Mobile

Wakati Simba Anajitafuta, Yanga Bingwa Msimu Huu....Hakuna Ushindani....

Yanga Bingwa Msimu Huu....Hakuna Ushindani....

Katika msimu huu wa Ligi Kuu ya NBC, tumeshuhudia jambo moja likijitokeza kwa uwazi—kushuka kwa viwango vya ushindani miongoni mwa timu zinazopaswa kuwa wapinzani wa kweli wa bingwa mtetezi, Yanga SC.

Yanga, ikiongozwa na kocha Nasreddine Nabi kwa mafanikio yaliyopita na sasa ikisukumwa na benchi jipya la ufundi, imeendelea kuonyesha nidhamu ya kiuchezaji, uimara wa kikosi na utulivu mkubwa wa kiutawala. Matokeo yake yamekuwa ya kuridhisha kwa mashabiki wao, lakini kwa upande wa upinzani wa ligi, hali hiyo imeacha maswali mengi.


Timu kama Simba SC, ambayo kihistoria imekuwa mpinzani mkuu wa Yanga, msimu huu imekuwa na wakati mgumu mabadiliko ya benchi la ufundi, majeraha kwa baadhi ya wachezaji tegemeo, pamoja na sintofahamu ya ndani ya kikosi imeonekana kuwaathiri moja kwa moja.


Hali ni hiyo hiyo kwa Azam FC ambao licha ya uwekezaji mkubwa, bado wanaonekana kukosa uthabiti wa kupata matokeo muhimu dhidi ya timu kubwa na zile ndogo.

Kwa hali ilivyo sasa, huwezi kujizuia kujiuliza: Je, msimu huu utamalizika bila kumpata mpinzani wa kweli wa Yanga? Na je, hii inaashiria tatizo kubwa zaidi la msingi kwenye maendeleo ya soka letu la ndani?

Ni wazi kuwa mashabiki wengi walitarajia ushindani mkali hadi dakika ya mwisho wa msimu, lakini dalili zinaonyesha Yanga anaweza kutetea ubingwa wake kwa mtindo wa "walk in the park".


Na kwa hakika, hili si jambo linalowafurahisha tu mashabiki wa Yanga, bali linaacha pengo la burudani na mvuto wa ligi kwa ujumla.


Kwa sasa, timu zingine hazina budi kujipanga upya si kwa ajili ya kumaliza msimu, bali kwa kutengeneza msingi imara wa kuwa wapinzani halisi msimu ujao, Ligi inahitaji timu zenye ushindani wa kweli, vinginevyo tutabaki na ligi ya klabu moja.'' @tingmugoa


JE ATATWAA UBINGWA BILA KUPIGWA???

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad