Manchester United wanafikiria kuwa na mpango wa kubadilishana wachezaji utakaomhusisha Marcus Rashford na mshambuliaji wa Aston Villa Ollie Watkins, Alexander Isak anatazamiwa kusalia Newcastle United na Manchester City wanapanga kumnunua mlinda mlango Diogo Costa.
Manchester United wanafikiria kuwa na mpango wa kubadilishana wachezaji ambao utamhusisha mshambuliaji Marcus Rashford, 27, wa kubadilisha uhamisho wa mkopo wa Aston Villa kuwa wa kudumu huku mchezaji mwenzake wa kimataifa wa Uingereza Ollie Watkins, 29, akijiunga na Man Utd wakati wa dirisha la uhamishaji wa majira ya joto. (Star)
Kipa wa Cameroon Andre Onana, 29, ataruhusiwa tu kuondoka Manchester United ikiwa klabu hiyo itapokea ofa ya zaidi ya £20m. (Mirror)
Kocha wa Atletico Madrid Diego Simeone anamfuatilia kwa karibu beki mwenzake wa kati wa Argentina na Tottenham Cristian Romero na huenda akajaribu kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kabla ya Kombe la Dunia la Vilabu msimu huu wa joto. (Sunday Express)
Winga wa Uhispania Nico Williams, 22, amehusishwa na kuhamia Arsenal na Barcelona lakini amependekeza kuwa anataka kusalia na Athletic Bilbao na kuichezea katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao ikiwa watafuzu. (AS - in Spanish)
Viktor Gyokeres wa Sporting anaaminika kuvutia vilabu kadhaa lakini mshambuliaji huyo wa Sweden mwenye umri wa miaka 26 anasema "hakuna anayeweza kutabiri kitakachotokea - tunafurahia wakati uliopo". (Metro)
Real Madrid wamepanga kuachana na kocha Carlo Ancelotti na wamewasiliana na kambi ya kocha wa Bayer Leverkusen Xabi Alonso, ingawa Mhispania huyo anaweza kuwagharimu takriban pauni milioni 15 kama malipo yake. (Sky Sports Germany)
Iwapo Ancelotti ataondoka Real Madrid angependelea kuchukua nafasi ya kocha wa timu ya taifa ya Brazil. (Athletic - subscription required)
Mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, ambaye anahusishwa na Arsenal na Liverpool, anatarajiwa kusalia Newcastle United huku Magpies wakipanga kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 katika uhamisho wa majira ya msimu wa joto. (Football Insider)
Chelsea, Newcastle na Juventus wanavutiwa na beki wa kati wa Korea Kusini Kim Min-jae, huku Bayern Munich wakiwa tayari kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports Germany)
Manchester City wanapanga kumnunua mlinda mlango wa Porto Diogo Costa na wanaamini kwamba ofa ya pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno inaweza kutosha, licha ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kuwa na kipengele cha kumnunua cha pauni milioni 63 katika mkataba wake. (Mirror)
Bayern Munich wanamfuatilia kiungo wa kati wa Chelsea na Brazil Andrey Santos, ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Strasbourg ya Ufaransa. (Mail)