SIMBA Nao Wajikusanya Watuma Offer Hii Kwa Fei Toto.....
Simba inamtaka Fei Toto na ile kauli ya kocha wao Fadlu alipozungumza mara baada ya mchezo wa robo fainali ya pili dhidi ya Al Masry, aliposhindwa kuficha siri ya kambi, akifichua kwamba klabu hiyo ipo kwenye mawindo ya kuwania saini ya kiungo namba 10 bora Tanzania, ambaye duru zinasema ndo Mzanzibar huyo.
.
Wekundu hao kwenye hesabu zao mpaka sasa, ingawa hawajaifuata rasmi Azam lakini imempa ofa kiungo huyo ya Sh 800 milioni na mshahara mkubwa usiopungua Sh30 milioni kwa mwezi.
.
Simba pia inajipanga kuishawishi Azam, iwachukue wachezaji wawili ndani ya dili hilo akiwamo winga mmoja na kiungo wa kati mmoja wote wazawa ukiweka mbali na fedha za kununua mkataba wake, lakini wekundu hao wanaona uzito kutoa kiasi cha Sh1 bilioni kumaliza dili hilo.
.
Wekundu hao wanatafuta saini ya Fei Toto, ikiwa ni kutamani kiungo namba 10 bora zaidi, ikiona kama staa wao msimu huu Jean Charles Ahoua licha ya kuongoza kwa kufunga mabao kwenye ligi na hata klabuni kwake akiwa na mabao 12, bado hawapi kitu kikubwa wanachotamani hasa kwenye mechi kubwa..
ya Watuma Offer Hii Kwa Fei Toto.....