WANANCHI, Young Africans Sc wamefuzu kwenda nusu fainali ya kombe la Muungano 2025 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya KVZ Fc ya Zanzibar katika uwanja wa Gombani, Pemba Zanzibar kwenye mchezo wa robo fainali uliofanyika leo Aprili 26, 2025.
FT: KVZ 0-2 Yanga
⚽ 28’ Aziz Ki
⚽ 88’ Nkane
Kiungo wa Young Africans Sc, Mudathir Yahya amechaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo na kuzawadiwa shilingi 200,000/ kutoka City Institute of Health Dar es Salaam.