KenGold Yawasimamisha Kazi Wachezaji Hawa



TAARIFA zinabainisha kuwa, siku chache baada ya KenGold kushuka daraja, imewasimamisha baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho na kocha wao wa viungo ikidaiwa ni kutokana na sababu za kinidhamu.

KenGold ambayo imeshiriki Ligi Kuu msimu huu kwa mara ya kwanza, imekuwa timu ya kwanza kushuka daraja baada ya kufungwa 2-1 na Coastal Union Jumatatu wiki hii ikibaki na pointi 16 ambazo haziwezi kuwafanya kutoka ndani ya na-fasi mbili za chini katika mechi tatu zilizobaki.

Wanaotajwa kusimamishwa ni Seleman Bwenzi, Abdallah Masoud ‘Cabaye’, Steven Duah, James Msuva na Uhuru Seleman ambaye ni kocha wa viungo.

Akizungumza, Cabaye ambaye ni miongoni mwa waliosimamishwa, amekiri kusimamishwa kwake kumetokana na utovu wa nidhamu. “Nilipishana kidogo na viongozi kwa sababu ya mambo fulani ambayo ni haki yangu lakini hawakunipatia kwa wakati, hivyo nilichoka kama binadamu ndio tukapishana.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad