KIKOSI cha Azam kipo katika mji wa Wasomi, Manispaa ya Bukoba kwa ajili ya mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, lakini kikiwa na pigo baada ya kiungo mshambuliaji nyota, Feisal Salum ‘Fei Toto’ kutokuwepo kutokana na kuwa majeruhi, huku kocha akidai kuvurugwa kwa kumkosa.
Inaelezwa nyota huyo anayeongoza kwa asisti katika ligi akiwa nazo 13 ameshindwa kuambatana na timu kwa sababu ya kuwa na maumivu ya mguu, jambo lililomfanya kocha Rachid Taoussi kujipanga upya jeshi aliloenda nalo ugenini ili kukamilisha lengo la kuondoka na pointi tatu muhimu.
."Fei amepata maumivu ya mguu, ila naamini atakuwa sawa hadi pale tutakaporejea ili aweze kujiandaa mechi muhimu zijazo, zikiwamo za michuano ya Kombe la Muungano na zile za Ligi Kuu." Alisema Taoussi.