Mobile

EDO Kumwembe: FEISAL Salum Atafika Akiwa Hoi Saana

Edo Kumwembe vs Feisal Salum


 EDO KUMWEMBE🎙FEISAL ATAFIKA AKIWA HOI SAANA

💬 Na kama kuna mwanadamu ambaye atakuwa analala hoi basi ni Feisal Salum, ‘Fei Toto’. Namna ambavyo siku yake nzima inaambatana na mambo mawili. Jambo la kwanza ni kufanya mazoezi au kucheza mechi. Jambo la pili ni kusoma ushauri wa kwenda Simba au kurudi Yanga.

Ukienda mitandaoni kuna mambo mawili. Lazima kurasa za wanahabari zimhusishe kwenda Simba au kurudi Yanga. Lakini hapo hapo lazima katika kurasa yake mwenyewe hata akiweka picha yake binafsi katika maisha yake binafsi, lazima maoni ya wengi katika picha hiyo ni kumtaka aende Simba au Yanga.Lazima Fei atakuwa amelala akiwa hoi. Lazima.

Kwanini hii inatokea? Ni kwa sababu Watanzania hawaamini kwamba mchezaji mkubwa kama Fei anaweza kuondoka timu kama Yanga au Simba akiwa katika ubora wake na kwenda kucheza Azam. Iliwahi kutokea kwa Mrisho Ngassa na hali ilikuwa kama hivi. Wakati ule hakukuwa na mitandao, lakini kila mahali ulikuwa ukikaa unaambiwa namna ambavyo watu wa Yanga walikuwa wanamtaka arudi. Ilikuwa presha kubwa kutoka katika magazeti na vijiwe vya kahawa.

Zaidi ya hili ni kwamba NYOTA ya Fei imeendelea kung’ara akiwa na Azam. Kuna wale wataalamu wa kumuombea mchezaji mkubwa mabaya pindi anapoondoka na kuendelea kucheza hapa hapa nchini. Kwa Fei jambo hili LIMEKWAMA kwa sababu Fei ameendelea kuwa Fei yule yule tu. Ameendelea kuwa mtamu kama alivyo na KIWANGO chake kimeendelea kuwa juu. Anafunga mabao, anasaidia timu yake kufunga mabao katika kiwango kile kile ambacho alikuwa nacho wakati akiwa Yanga.

Simba na Yanga ni wabinafsi. Hawataki timu nyingine yoyote iwe kubwa nje ya wao. Zamani kidogo kulikuwa na simulizi ya uongo kwamba mashabiki wangependa zitokee timu nyingine kubwa zianzishe upinzani kwa Simba na Yanga. Kumbe mashabiki waliokuwa wanasema hivi walikuwa wanazidanganya nafsi zao.

Fei kwenda Azam ilileta chuki kutoka kwa mashabiki wa Yanga. Mchezaji wa Azam akienda Yanga haina shida. Mchezaji staa wa Yanga akienda Azam inaleta chuki. Jiulize kwanini Prince Dube hatazamwi kwa jicho la chuki.”

— Edo Kumwembe [Mwanaspoti]

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad