Mobile

CAF Yafanya Mabadiliko ya Ghafla Mechi ya Simba na Stellenbosch




Shirikisho la Soka barani Afrika CAF limefanya mabadiliko ya ghafla ya mwamumuzi wa mchezo wa mkondo wa pili wa nusu fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji Stellenbosch na Simba SC. Kulingana na taarifa tulizozipata hivi sasa mechi hiyo itachezwa tarehe 27 Aprili 2025.

CAF imetangaza mwamuzi Maarouf Eid Mansour kutoka Misri alichukua nafasi ya Amin Omar kutoka Misri ambaye hapo awali alipangwa kuchezesha mechi hiyo. Sababu ya Mabadiliko hayo ya ghafla haijabainika.

Aidha mwamuzi Mansour atasaidiwa na wenzake kutoka Misri ambao ni Mahmoud Abouelregal na Ahmed Ibrahim ambao tangu awali walipangwa kuwa wasaidizi lakini pia kuna mabadiliko ya refa wa akiba ambao sasa atakuwa Mahmoud Nagy naye kutoka Misri.

Bechir Hassan kutoka Tunisia atakuwa Mtathmini wa marefa huku Kamishna wa mchezo huo akiwa Kelesitse Gilika wa Botswana. Hakuna mabadiliko upande wa marefa wanaosimamia teknolojia ya video ya usimamizi kwa marefa VAR ambapo Kuna Mahmoud Ashour Mahmoud Elbana kutoka Misri.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad