Mobile

Azam Waweka Kitita Kwa Feitoto Lakini Wapi, Yanga na Simba Waingia Vitani

Azam Waweka Kitita Kwa Feitoto Lakini Wapi, Yanga na Simba Waingia Vitani


VITA mpya kwa Simba na Yanga ni namna zinavyopambana kuonyeshana jeuri ya fedha, kumshawishi kiungo wa Azam, Feisal Salum ‘Fei Toto’, zikimtengea mamilioni ya kufuru kwa ofa tofauti lakini pia ipo klabu moja ya Sauzi

Tuanze na Ofa ya Klabu yake kwanza. Fei Toto mkataba wake na Azam, umebakiza mwaka mmoja na miezi kadhaa, ambapo msimu huu utakapomalizika, atakuwa amebakiza mwaka mmoja kamili lakini matajiri hao wa Chamazi inaelezwa wameshamuahidi ofa ambayo HAKUNA klabu yoyote ya Tanzania ina uwezo wa kumpa, ingawa bado hajamwaga wino.

Lakini Azam, imekumbana na kigingi baada ya kiungo huyo, KUGOMA kukubali kuongeza mkataba, akiwaambia mabosi wake kwamba ana kiu ya kwenda nje ya nchi kujaribu maisha ya soka. Hata hivyo, mbali na Fei Toto kutoa sababu hiyo, Arena tunafamu kwamba, kiungo huyo hana shida na namna anavyohudumiwa kifedha na matajiri hao, lakini changamoto kubwa ni ubora wa kikosi chao kiushindani, akiona kama anachelewa kuwa mchezaji mkubwa zaidi.

Azam imemuwekea ofa Fei Toto, yenye thamani ya zaidi ya Sh 900 milioni, ikiwamo nyumba 🏠 gari ya kisasa zaidi tofauti ile Toyota Harrier  aliyopewa wakati anasaini mkataba wa sasa na zaidi ni kuboreshwa kwa maslahi yake. Matajiri hao, sio tu kwamba wanataka kumbakisha Fei Toto bali namba zake zinawashawishi ambapo licha ya kukosa kiatu cha ufungaji bora kwenye ligi msimu uliopita, aliibuka kuwa mfungaji bora ndani ya klabu yake, akiwa na mabao 19 akizidiwa mabao mawili na mfungaji bora kwenye ligi kiungo wa Yanga, Stephanie Aziz KI.

Msimu huu, bado Fei Toto ameendeleza ubora wake kiutofauti, akihusika kwenye mabao 17, akifunga manne na kutoa asisti 13, na hivyo kuwa kinara wa kupika mabao kwenye ligi akiwa amebakiza mechi nne kumaliza msimu.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad