Suala la Kocha Gamondi Kutua Singida Black STARS, Ishu Nzima Iko Hivi.....

Suala la Kocha Gamondi Kutua Singida Black STARS, Ishu Nzima Iko Hivi.....


UONGOZI wa Singida Black Stars upo hatua ya mwisho ya kumalizana na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Miguel Gamondi ili kuchukus mikobs iliyochwa na Patrick Aussems ‘Uchebe’.

Uchebe alisimamishwa kazi kwa kuvunjiwa mkataba na Singida baada ya matokeo mabaya mfululizo akianza na kichapo na Yanga bao 1-0 na sare mfululizo dhidi ya Coastal Union na Tabora United na kwa sasa timu hiyo ipo chini ya Mkurugenzi wa Ufundi, Ramadhan Nsanzurwimo na David Ouma.

Habari zilizonaswa ni kwamba Singida ipo katika hatua nzuri ya mazungumzo kumalizana na Gamondi aliyeondolewa Yanga akiwa ameweka rekodi mbalimbali katika Ligi Kuu na michuano ya CAF kwa klabu hiyo kongwe.

Chanzo cha kuaminika kutoka Singida, kimesema kuwa, mazungumo kocha huyo yapo pazuri na wale waliopo sasa watakuwa wasaidizi wa Gamondi mwenye uraia wa Argentina.

“Tunatambua ubora wa mbinu na CV kubwa ya Gamondi itakuja kuongeza thamani ya timu na kukuza vipaji vya wachezaji wetu ambao malengo yao makubwa ni kuipambania timu yetu kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Tuna matarajio makubwa kumpata kabla ya dirisha la usajili kufungwa ili apate nafasi ya kupendekeza usajili katika dirisha dogo la usajili linafunguliwa Desemba 15 hadi Januari 15 mwakani.”

Gamondi aliondolewa Yanga baada ya vipigo viwili mfululizo akianza na Azam FC 1-0, na kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Tabora United zote zikichezwa kwenye uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Akiwa na Yanga Gamondi ameongoza katika jumla ya michezo 40 ya Ligi Kuu kuanzia msimu wa 2023-2024, hadi huu wa sasa wa 2024-2025 ambapo alishinda 34, sare minne na kupoteza pia mara nne, huku timu hiyo ikivuna jumla ya mabao 85 na kufungwa 18 tu na kukusanya pointi 104 hadi alipoondolewa Jangwani.

Pia kocha huyo ametwaa mataji matatu likiwamo la Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho msimu uliopita pamoja na Ngao ya Jamii iliyobeba msimu huu, mbali na kuifikisha timu makundi ya Ligi ya Mabingwa mara mbili mfululizo ikiwa ni rekodi kwani mara mwisho kutinga hatua hiyo ilikuwa miaka 25 iliyopita.

Gamondi aliifikisha Yanga hadi robo fainali ya michuano hiyo ya CAF na kung’olewa kwa penalti na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini huku bao halali la Stephane Aziz Ki likikataliwa kitatanishi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad