Haji Manara Aibua Mazito Yanga, Kocha Gamondi Atajwa



Haji Manara Aibua Mazito Yanga, Kocha Gamondi Atajwa

DAR ES SALAAM: HAJI Manara amenukuliwa akisema kocha wa Yanga Miguel Gamondi ni mtu anayependa vijimaneno maneno ambavyo havina afya katika maisha akieleza kuwa vijajenga chuki baina ya watu.

Akizungumza katika kipindi cha Ampilifaya na Millard Ayo Manara amesema moja ya watu ambao hawakupenda yeye kurejea katika majukumu yake baada ya kumaliza adhabu ni kocha Miguel Gamondi.

“Gamondi ana changamoto zake tulikuwa tunajiandaa na siku ya wananchi ilikuwa ni tarehe tatu nikawaambia wenzangu kuwa natamani nikaongeee na wachezaji ili wajue ambacho tumepanga kukifanya siku ya Mwananchi,

Nilivyofika wote walifurahia ila Gamondi hakuwa ‘happy’ na hakuweza kujizuia akanifuata akaniambia nasikia wewe umepost kuwa unataka mimi nifukuzwe. Nilishangaa sanaa maana sikuwahi kufanya hivyo, nikamuulia umetoa wapi huo uongo”, amesema Manara na kuongeza kuwa

Siku moja nilikutana nae kwenye ‘lift’ sikumsalimia mimi siwezi kuwa mnafiki japo namuunga mkono kwenye kazi yake kwasababu ni kocha mzuri na ana mbinu nzuri”

Kauli za Manara zimepata nguvu wakati huu kocha Gamondi akitajwa kuwa muda wowote atafutwa kazi klabu hapo kutokana sababu lukuki huku misimamo yake mikali ikitajwa kuongoza chati ya sababu ya kunyolewa.

Manara ameongeza kuwa kwa sasa hana ukaribu na Rais wa Yanga Hersi Said kama zamani.

“Tuna miezi zaidi ya miwili hatujawasiliana, ninaweza kukuambia kuwa hapo awali tulikuwa tukipigiana simu kwa siku hata mara 30, yaani familia yangu na yake ilikuwa ni kitu kimoja, ujue inabidi mtu atambue thamani yako kwanza, huwezi kulazimisha mtu kuujua umuhimu wako amesema”, Manara

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad