Bodi ya klabu ya Zamalek Sc inazidi kufanya majadiliano ya kina zaidi kuhusu kumsajili beki wa zamani wa Rela Madrid na sasa Spain,Bodi ya Zamalek inaendelea kujadili kuhusu mshahara ambao Sergio Ramos alihitaji ili kuichezea Zamalek.
Ahmed Shawky ambae ni mratibu,Ofisa habari wa klabu ya Zamalek amethibitisha taarifa hio ya usajili wa nyota huyo wa Spain na Real Madrid Sergio Ramos ni kweli kabisa.
Sergio Ramos kwasasa ni mchezaji huru mara baada ya kumaliza mkataba wake na Sevilla msimu uliopita,kwasasa Zamalek wanachojadili ni uwekezaji wa mshahara ili kumlipa Sergio Ramos ili asaini mkataba.