RC Chalamila atangaza wiki ya Muungano

RC Chalamila atangaza wiki ya Muungano

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila ametangaza wiki ya Muungano kuelekea kilele Miaka 60 tangu Tanganyika na Zanzibar kuungana

Wiki yakuelekea Tarehe 26.4.2024 siku ambayo kilele cha maadhimisho ya Miaka 60 Tangu Tanganyika na zanzibar zilipoungana ambapo yatafanyika katika Viwanja vya Uhuru jijini Dar es salaam huku Mgeni rasmi akitarajiwa kua Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan

Mkuu wa mkoa amesema ratiba itaanza saa 12 Alfajiri na Ifikapo saa moja viongozi na watanzania wote watawasili kwa utaratibu maalum viwanjani hapo

Wakati huohuo Mkuu wa mkoa amesema kesho April 25 viwanja vya Tanganyika Packers, Kutakua na Tamasha kubwa kuelekea kilele cha miaka 60 ambapo Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dotto Biteko atakuepo kama Mgeni Rasmi na Wasanii kama Diamond Platnumz na Zuchu watakuepo ,

Amesema Tamasha hili ni kuanzia saa 11 jioni na hakuna kiingilio huku ikifika saa tatu Usiku kupitia Luninga na Watanzania watakaokuepo hapo Mhe.Rais Dokta Samia Suluhu Hassan atahutubia

"Hakutakua na kiingilio cha aina yoyote ,Wasanii wakubwa wote watakuepo hali ya usalama itakua ni kubwa kwaio watu wasiogope lakini pia kutakua na hotuba ya Mhe.Rais ikifika saa tatu Usiku "Mkuu wa mkoa

Aidha ,Mkuu wa mkoa amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi viwanja vya uhuru na wajikite zaidi kuangalia manufaa na sio mapungufu madogo madogo ya Muungano

"Tujikite zaidi kuangalia manufaa ya muungano kuliko kujikita kwenye Dosali ndogo ,Muungano una manufaa kwasababu umepanua wigo wa Taifa letu katika sekta za kimataifa ,Wigo wa lugha ya kiswahili lugha imekua kibiashara kwa kuuza bidhaa lugha katika mataifa mengine,Wigo katika sekta ya utalii kwa wageni kuja Bara na Visiwani "

"Naomba nichukue nafasi hii kuendelea kuwakaribisha makundi yote,Watumishi wote wa umma,Vyama vya wafanyakazi,Machinga na makundi yote yaliyopo ndani ya mkoa wa Dar es salaam tujitokeze uwanja wa Uhuru ,Vyombo vyetu vyote vya usalama vitahakikisha kutakuepo na usalama "Amesema Mkuu wa Mkoa


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.