LAANA MBAYA YA YANGA YAFANYA MAZITO…NI BAADA YA AZIZ KI KUFANYA HAYA…ISHU NZIMA IPO HIVI A-Z

 LAANA MBAYA YA YANGA YAFANYA MAZITO…NI BAADA YA AZIZ KI KUFANYA HAYA…ISHU NZIMA IPO HIVI A-Z

Huko Afrika Kusini kwenye Uwanja wa Loftus Versfeld mjini Pretoria, Mamelodi Sundowns ilishindwa kutumia vyema fursa ya kucheza nyumbani dhidi ya Esperance na kuchapwa 1-0 na kusukumwa nje ya michuano hiyo kwa jumla ya mabao 2-0, kufuatia kichapo cha bao 1-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika Tunisia.

Mchezo huo ulisimama kwa dakika kadhaa baada ya mvua kubwa kunyesha ikiambatana na radi na kusababisha taa uzima uwanjaji hapo jambo lililosababisha mchezo huo kusimama baadae hali ilivyorejea vizuri mechi ikaendelea.

Rayed Bouchniba niye aliyewazima Mamelodi kwao kwa bao safi la kipindi cha pili na hivyo kuhitimisha safari ya Wasauzi hao kwenye michuano hiyo baada ya kuvuka kwa kutata kwenye robo fainali dhidi ya Yanga ya Tanzania kwa mikwaju ya penati baada ya kukataliwa kwa bao la Stephanie Aziz Ki.

Huko Loftus Versfeld, Mamelodi ilimiliki mpira kwa asilimia 72 na kupiga mashuti 27, huku sita yakilenga goli, wakati Esperance ilimiliki mpira kwa 28 na kupiga mashuti sita, matatu tu ndiyo yaliyolenga goli na moja likitinga nyavuni.

Mamelodi ilipiga pasi 491 na zilizokuwa sahihi ni 385, huku Esperance ilipiga pasi 208 na pasi 102 zikiwa sahihi.

Mamelodi tangu ameingia robo fainali hajafunga bao hata moja mpaka ametolewa nusu fainali. Mechi mbili za Yanga kwenye hatua ya robo fainali alitoa sare ya bila kufungana ugenini na nyumbani, mechi za nusu fainali dhidi ya Esperance amefungwa mechi zotembili, ugenini 1-0 na nyumbani 0-1.

Mechi ya kwanza ya fainali itapigwa Jumamosi, Mei 18 kwa Esperance kuwa mwenyeji huko Tunisia, wakati ya pili itapigwa, Jumamosi, Mei 25 huko Misri, ambapo Al Ahly itakuwa wenyeji. 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.