Kocha Gamondi Atamba Kwa Namna Hii, Awachungulia Mtibwa Kisha Awatumia Salamu Hizi

 

Kocha Gamondi Atamba Kwa Namna Hii, Awachungulia Mtibwa Kisha Awatumia Salamu Hizi
Kocha Gamondi 

Kocha Gamondi Atamba Kwa Namna Hii, Awachungulia Mtibwa Kisha Awatumia Salamu Hizi

Kocha Mkuu wa Young Africans Miguel Gamondi amemjibu Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar Zuberi Katwila, kwa kusema hasira zake zote atazihamishia katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaowakutanisha na Wakata miwa hao kutoka Manungu, Tuariani mkoani Morogoro.

Kauli hiyo imekuja kufuatia tambo za Kocha Katwila kuelekea mchezo huo wa Ligi Kuu utakaopigwa Jumamosi (Desemba 16), ambapo amesema atahakikisha anafufukia mbele ya mabingwa hao watetezi, baada ya kupoteza michezo mitano mfululizo.

Gamondi amesema kuwa wameuweka kando mchezo wao wa marudiano dhidi ya Medeama SC na sasa akili zao wanazielekeza mechi na Mtibwa Sugar ambao upo mbele yao.

Gamondi amesema kuwa anaamini kikubwa wanarejea katika ligi, kwa lengo moja pekee ambalo kushinda kila mchezo uliokuwepo mbele yao, kwa kuanza dhidi ya Mtibwa Sugar.

Ameongeza kuwa, baada ya mchezo dhidi ya Medeama SC, alifanya kikao na wachezaji wake, kuwataka kusahau matokeo hayo ya sare ya bao 1-1 waliyoyapata na badala yake waelekeze akili na nguvu zao katika ligi watakapocheza na Mtibwa Sugar.

“Kila mchezo tunauchukulia umuhimu mkubwa, na kikubwa ni kupata ushindi na siyo kitu kingine, ninaheshimu kila mpinzani nitakayekutana naye mbele katika ligi na mashindano ya kimataifa.

“Wachezaji nimewaambia wasahau matokeo ya Medeama SC, na badala yake tunelekeze nguvu katika michezo ya ligi, tutakaoanza kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar.

“Ninataka kuona tunaendelea na kasi ya ushindi mkubwa na soka safi la kuvutia, kama tulivyoanza katika michezo ya awali ya ligi ambayo tulipata ushindi na soka safi litakalowafuraisha mashabiki wetu,” amesema Gamondi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.