Clatous Chama Asimamishwa Simba Kwa Utovu wa Nizamu
Vongozi wa klabu ya Simba umewasimamisha wachezaji Nassor Kapama na Clatous Chama kutokana na vitendo vya utovu wa nidhamu.
Taarifa iliyotolewa na Klabu ya Simba imeeleza kuwa kufuatia vitendo hivyo wachezaji hao watapelekwa katika kamati ya nidhamu kwa hatua zaidi za kinidhamu.
Aidha uongozi wa klabu ya Simba umesisitiza kuwa watumishi wake wote wanapaswa kuzingatia misingi ya maadili na nidhamu kwani klabu hiyo haitasita kumchukulia hatua yeyote atakaethibitika kwenda kinyume na utaratibu huo.