Simba Wafunguka UKWELI Mchungu Kuhusu usajili wa Luis Miquissone
Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu amesema klabu hiyo bado haijamsajili aliyekuwa winga wa klabu hiyo Luis Jose Miquissone (27) japo Simba SC inawasiliana tu na nyota huyo raia wa Msumbiji anayekipiga katika klabu ya Al Ahly ya Misri.
"Luis Miquissone anaipenda Simba na hata Mashabiki wa Simba wanampenda sana ila niseme kweli hatujamsajili japo tunawasiliana tu,” amesems Murtaza Mangungu.
Miquissone ni kiungo mshambuliaji aliyeitumikia Simba kwa mafanikio makubwa kabla ya kuuzwa na kutimkia Al Ahly ya Misri ambako alicheza msimu mmoja kisha kupelekwa Uarabuni kwa mkopo kabla ya kurejea nyumbani kwao Msumbiji ambako yupo mpaka sasa.
Fundi huyo wa boli ni miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kujiunga na Simba katika dirisha hili kubwa la usajili