Mchezaji Jonas Mkude Afichua SIRI Nzito Jezi Namba 20

 

Mchezaji Jonas Mkude Afichua SIRI Nzito Jezi Namba 20

Jonas Mkude ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Yanga ikiwa ni wiki chache tangu apewe 'Thank You' na Simba aliyoitumika kwa miaka 13, huku akipewa namba 20 aliyokuwa akiitumia akiwa Msimbazi, na imefichua sababu ya kiungo huyo kuikomalia namba hiyo.


Inaelezwa Yanga ilipanga kumpa Mkude jezi namba 6, lakini aliigomea namba hiyo kama ambavyo Mwanaspoti liliwahabarisha juzi baada ya mwenyewe kuikomalia jezi namba 20 na kwamba dili lake Jangwani lilikamilika kitambo, ishu ikawa ni namba ya jezi aliotakiwa kupwe.


Mtu wa karibu wa Mkude anayefahamikia zaidi kama Nungunungu, alisema jamaa alikataa kutumia namba nyingine, kwa vile namba 20 amekuwa akiitumia kwa muda mrefu na katika mitandao yake ya kijamii imekuwa 'verified'.


Kwa maana hiyo, Mkude ataendelea kutumia jezi namba 20 ambayo alikuwa anatumia Simba wakati uongozi ukiendelea kufanya mazungumzo na Zawadi Mauya, ambaye alikuwa anaitumia jezi namba 20 ili amuachie.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi, Mkude alisema anatamani iwe 'surprise' kwa mashabiki wake hivyo hawezi kusema ni namba ipi atatumia.


"Sitamani ifahamike mapema, Wananchi waje siku ya Mwananchi, Julai 22 nitakuwepo Uwanja wa Benjamin Mkapa," alisema Mkude.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.