Ahmed Ally: Inshu ya Sawadogo ni uzushi tu

Ismael Sawadogo


Uongozi wa Simba SC umefunguka kwa kina ishu la Kiungo Mkabaji kutoka Burkina Faso Ismael Sawadogo, ambaye anadaiwa kuugomea Uongozi wa Klabu hiyo kuvunjwa kwa mkataba wake, akishinikiza kulipwa Shilingi Milioni 700 kama fidia.


Sawadogo aliyesajiliwa Simba SC wakati wa Dirisha Dogo mwezi Januari 2023, amekuwa akitajwa kuwa katika orodha ya wachezaji wanaoachwa klabuni hapo katika kipindi hiki, japo Ungozi wa Simba SC haujawahi kuzungumza lolote kuhusu mpango huo.


Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC Ahmed Ally, amesema habari hizo hazina ukweli wowote zaidi ya kuzushwa katika mitandao ya kijamii kwa maslahi ya watu binafsi ambao wamepanga kuichafua klabu yao, hasa katika kipindi hiki.


Ahmed amesema mchezaji anaposaini mkataba na Simba SC kuna makubaliano yanakuwapo mwanzoni ya jinsi ambavyo akishindwa kuendelea kuitumikia klabu hiyo au viongozi wakihitaji kuvunja mkataba wanachotakiwa kukifanya kwanza.


Amesema Sawadogo ana mkataba wa mwaka mmoja na wako kwenye mazungumzo ya kutoendelea naye kwa msimu ujao na baada ya maafikiano ya pande zote mbili wataweka wazi kuachana naye rasmi.


Ahmed amesema Simba SC inaendeshwa kisasa katika mazungumzo hayo na si suala la fedha kwa sababu kabla ya kusaini mkataba kuna kipengele ambacho kiko wazi mchezaji au klabu atakapovunja mkataba na anapouzwa nini kifanyike kabla.


“Hayo masuala la Sh. milioni 700 sijui yametoka wapi kwa sababu kila kitu kipo wazi, ni kweli Sawadogo hatutaendelea naye kwa msimu ujao na tuko kwenye mazungumzo ya kuvunja mkataba wake,” amesema Ahmed.


Ameongeza kuwa suala la fedha ya kumlipa mchezaji halijadiliwi bali linakuwapo kwenye mkataba ambao wanaingia naye anaposaini kuitumikia klabu hiyo na hadi sasa hakuna mchezaji ambaye ameachana nao anayedai haki zake

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad