Wakati tetesi zikiendelea kuzagaa kila kona kuwa mastaa wa Simba wanatakiwa katika vilabu mbalimbali Afrika na hata Ulaya, Meneja wa Mawasiliano wa Klabu ya Simba Ahmed Ally ameibuka na kusafisha hali ya hewa.
Tetesi hizo ambazo nyingi zimewaacha Mashabiki na wapenzi wa Simba katika hali ya Sintofahamu ni kama zimekanushwa na Msemaji huyo wa Klabu ambapo kupitia kurasa zake za Mitandao ya Kijamii ameandika;
"Unapokua na wachezaji wenye Quality kubwa tegemea tetesi nyingi kipindi cha usajili
Mohammed Hussein anatakiwa na timu za South Afrika
Manula anukia Azam Fc
Baleke anatakiwa na timu za Ulaya
Niwathibitishie Wana Simba hakuna mchezaji ambae yupo kwenye mipango yetu ataondoka, Wale waliomaliza mkataba na tunawahitaji watasalia
Maboresho tunayoyafanya ni pamoja na kuwabakisha wale tunaowahitaji"