Msemaji wa Simba Ahmed Ally Amjibu Hans Rafael Sakata la Zimbwe



"Mdogo wangu Hansi Rafaeli nimeona andiko lako umenipopoa kuwa napambana kuzima utambulisho wa Zimbwe, kwakua umemtaja Zimbwe hili siwezi kujibu maana umemtaja mtu ninaemuheshimu na kumpenda sana.

Lakini kwakua umenivaa maungoni nami siwez kufunika kombe

Kwanza naomba nikuulize tuu hii vita ni yako binafsi au umetumwa na wale wanaoliliana harusini

Kama wamekutuma basi wamekubebesha mzigo mkubwa sana mdogo wangu

Hao wenzio wameshanishindwa hawaniwezi na wananiogopa kama Mjumbe wa CCM

Wameshanishtaki saaaana, Wamenishtaki TFF na nikawabwaga vibaya vibaya

Sasa wamekuongeza na wewe hakikisha umejipanga maana umekaa upande dhaifu

Kingine ninachoomba kujua tu unataka vita na mimi kama Mwandishi au Wakala mtiifu wa kikundi cha kuliliana harusini

Ni muhimu nijue haya ili nikishambulia nijue namshambulia adui wa aina gani?

Ukiwa unasimama kama Mwandishi basi niache kukushambulia maana kawaida yangu naheshimu sana Waandishi na tena naheshimu sana Media yako hivyo siwezi kukujibu.

Ila kama umekaa upande wa wapinzani wangu jipange mdogo wangu mimi sio mtu wa kawaida!!" Ameandika Msemaji wa Simba -Ahmedy Ally.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad