Kwa Kocha Folz Hakuna Timu Tanzania Itatamani Kukutana na Yanga

Kwa Kocha Folz Hakuna Timu Tanzania Itatamani Kukutana na Yanga


Achana na magoli ya Pacome,Boyeli na Nondo,achana na kasi ya umeme ya Ecua na Chikola ila naomba tuzungumzie “Romain Folz Ball”


Mechi ya kwanza ya ushindani ya Folz wote tumeiona,anataka timu yake iwe compact wakati wa kuzuia,na wakati wa kushambulia anahitaji kudumisha upana huku akiwataka mawinga wake (Pacome & Ecua) waanzie mikimbio pembeni kisha wafanye mikato ya haraka ya wembe kuingia kwenye box la timu pinzani (Razor-sharp movements).


Kati kati ya uwanja Folz anahitaji fluidity (Free flowing football) wale viungo watatu wanatakiwa kutengeneza umbo la pembe tatu (triangle) huku muda wote wakibadilishana nafasi….Folz anamtaka namba #6 kucheza kama namba #8 kisha namba #8 kuchezakama namba #10 na namba #10 kucheza kama namba #6. Wale watatu (Balla Conte,Maxi na Doumbia) wanabadilishana sana nafasi.


Tayari Idea ya Folz imeonekana kilichobaki ni kutafuta “Chemistry” baina ya mchezaji na mchezaji kitu ambacho nahisi kitachukua miezi miwili hadi mitatu baada ya hapo hakuna timu Tanzania itatamani kukutana na Yanga.


TF Rayon 1-3 Yanga.


Kombe la kwanza la wananchi kabatini📌

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad