Hatimaye Elie Mpanzu Awafunga Watu Midomo, Atinga Kambini Simba

Hatimaye Elie Mpanzu Awafunga Watu Midomo, Atinga Kambini Simba

Baada ya sintofahamu juu ya hatma ya winga Ellie Mpanzu ndani ya klabu ya Simba Sc huku tetesi zikimhusisha kujiunga na Yanga Sc hatimaye mzizi wa fitna umevunjwa baada ya nyota huyo kujiunga na kambi Simba Sc ya maandalizi ya msimu mpya huko Misri.

Nyota huyo raia wa DR Congo amejiunga na wachezaji wenzake waliopo mjini kambini lsmailia nchini Misri akitokea kwao alipokuwa mapumzikoni baada ya kumalizika kwa msimu wa 2024/25.

Taarifa ya Simba Sc imeeleza kuwa Mpanzu amechelewa kujiunga na timu kutokana na kuchelewa kupata vibali vya kuingia nchini Misri ambavyo kwa sasa vimekamilika na tayari amejiunga na kambi hiyo itakayodumu kwa wiki nne kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad