Edo Kumwembe: Hii Ndiyo Nguvu ya Siasa za Mpira Wetu Bongo

Edo Kumwembe: Hii Ndiyo Nguvu ya Siasa za Mpira Wetu Bongo


Haya mambo ya Conte ndiyo tuyapendayo. Tanzania mpira wetu kivyetuvyetu. Kuna viungo wakali Mali, Senegal, Ivory Coast, Ghana, Cameroon, Togo na kwingineko, lakini sisi lazima tunaipa dunia udogo kwa kufanya vita ya kugombania mchezaji mmoja. Baada ya hapo anayeshinda mbio anajitapa haswa.


Kando ya hapo rafiki yetu, Mwigulu Nchemba huwa anafanyiwa skauti nzuri na mtu fulani na mwishowe analeta vifaa vikali na wote tunabakia mdomo wazi. Katika dunia ambayo tunamgombania Conte kule Singida walikwenda sehemu na kuwapata kina Arthur Bada, Damaro Camara, Marouf Tchakei kimya kimya. Hata hivyo, ukimya huu wa Singida huwa hatuutaki. Sisi lazima tutiane kashikashi.


Kwa mfano, nilishangazwa niliposikia Conte haitaki Yanga licha ya Yanga kumalizana na klabu yake. Ghafla unamwona na tabasamu akiwa kando ya Hersi. Unajiuliza, stori ya yeye kutoitaka Yanga na ghafla akaibukia Salamander ilikuwa imelenga kuupa usajili huu nguvu kwamba Yanga walikuwa wamepindua meza kibabe?


Kinachotokea hapa ni mashabiki wengi wa Simba wameanza kunyong’onyea kabla ya msimu mpya haujaanza. Yanga wameanza kuwaua kisaikolojia kwa kuonyesha licha ya kuwa wao ni bora kwa sasa, lakini wataendelea kuwa bora zaidi kwa sababu wameinasa saini ya kiungo kama Conte.


Simba wananyong’onyea kama vile Conte ndiye kiungo bora zaidi wa chini aliyebakia katika soka la Afrika. HII NDIYO NGUVU YA SIASA ZA MPIRA WETU. Watu wataanza kuwatukana viongozi wa timu kwa kuonekana ni wazembe au wana mchakato mrefu wa kutoa pesa kunasa wachezaji. Mpira wetu kivyetuvyetu. .


Kitu kibaya zaidi ni hata maofisa wa timu huwa wanaingia katika mtego huu wakati wa usajili. Nadhani Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally hakupaswa kumzungumzia Conte alipoulizwa na waandishi wa habari wa redio mbalimbali nchini. Mfano ni pale alipokiri Simba walikuwa wanamhitaji Conte. Hakukuwa na umuhimu.

.

Ofisa anayehusika na timu anapaswa kutoa kauli za kidiplomasia bila ya kutaja jina la mchezaji hata kama akibananishwa. Ni kazi ya waandishi wa habari kupekua kadri wawezavyo, lakini kiongozi hapaswi kuthibitisha. Kama inatokea kushindwa kama hivi unaiweka klabu katika sehemu salama mbele ya mashabiki.” — Legend Edo Kumwembe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad