Anaandika Ahmed Ally✍️
Tuna kila sababu ya kujipongeza kwa maamuzi sahihi tuliochukua kwa Nahodha wetu kipenzi Mohamed Hussein
Kwanza ifahamike kuwa tunampenda, tunamheshimu na hiyo itabaki milele
Ulikua ni muda sahihi wa Tshaba kuondoka Simba na muda sahihi wa Simba kuachana na Tshaba
Kwenye hili agano sio Simba sio Tshaba ambae amepata hasara kila mmoja amenufaika na maamuzi haya
Kwa sasa wataibuka wengi kulaumu lengo lao kuonesha kuwa Simba tumekosea pili kuwapa faraja waliomchukua na tatu ni kutufinitisha sisi na Tshaba pamoja na mashabiki
Ukweli ni kwamba tumepoteza aliyewahi kuwa mchezaji wetu bora sana
Miaka mitatu nyuma mchezaji wetu mmoja ambae pia alikua Nahodha alimaliza Mkataba, Viongozi wakaona taabu kumuachia kutokana na heshima yake tukamuongezea Mkataba wa miaka miwili
Kilichofuatia miaka yote miwili alikaa Benchi na kama haitoshi zipo nyakati alisumbuliwa na Majeraha na akaacha kucheza na akaenda kufundisha timu ya vijana akiwa bado ana mkataba wa Uchezaji
Hayo yote yalitokea kwa sababu hatukutaka kuupokea ukweli kuwa muda wake uliisha tukabaki nae kwa sababu historia na heshima
Ndugu zangu Wana Simba kwa hili tutembee kifua mbele tumefanya maamuzi kwa kuangalia Simba bora ya keshoWala tusiingie ubaridi kwa kua anaenda upinzani wameshaenda wengi na hakuna maajabu
Muhimu sasa ni kuwahimiza Viongozi wetu kusajili mchezaji mwingine kama Tshabalala au zaidi ya Tshabalala
Na hapo sina shaka na viongozi wetu watafanya hilo kwa sababu maandalizi yalishafanyika muda mrefu
Kila la heri Captain @official_mohamedhussein15 Mungu akusimamie, Sisi tunakupenda sana
Wana Simba tusonge mbele mpaka tuko salama kwa sababu hakuna kinachotokea bahati mbaya!!!