CAF Yatangaza Vilabu 75 Bora Afrika 2025, Klabu 3 za Tanzania Zatamba

 

CAF Yatangaza Vilabu 75 Bora Afrika 2025, Klabu 3 za Tanzania Zatamba

Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) leo limetoa orodha ya vilabu 75 bora kwa mwaka 2025, ikizingatia viwango na alama walizokusanya kutokana na ushiriki wao katika mashindano ya CAF na michuano mingine mikubwa barani.


Kwa upande wa Tanzania, Simba SC imeorodheshwa kwenye nafasi ya tano ikiwa na alama 48, ikithibitisha nafasi yake kama moja ya nguvu kubwa za soka barani. Yanga SC imechukua nafasi ya 12 kwa alama 34, ikiendelea kudhihirisha ushindani wake katika ngazi ya kimataifa.

Namungo FC nayo imetajwa kwenye nafasi ya 75 ikiwa na alama 0.5, ikiwa ni matokeo ya ushiriki wake katika mashindano ya kimataifa katika kipindi kilichopita.


Orodha hii ya CAF hutolewa kila mwaka na hutumika kama kipimo cha maendeleo na ushindani wa vilabu barani Afrika

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad