Mobile

Yanga Yapanga Kumwongeza Aucho kwa Mwaka Mmoja Zaidi

 

Yanga Yapanga Kumwongeza Aucho kwa Mwaka Mmoja Zaidi


Kiungo mkabaji wa Klabu ya Yanga SC, Khalid Aucho, yuko mbioni kuongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Jangwani kwa msimu wa 2025/26.


Aucho, ambaye alikuwa sehemu ya kikosi cha kwanza kilichosaidia Yanga kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2024/25, alicheza mechi 22 kati ya 30, akicheza jumla ya dakika 1,735 kati ya 2,700 zilizowekwa kwa ligi hiyo.


Katika mafanikio hayo, Aucho alihusika moja kwa moja kwenye mabao 2 kati ya 83 yaliyofungwa na Yanga kwenye ligi – akifunga bao moja na kutoa pasi ya bao moja (assist).


Mkataba wake wa awali umemalizika mwishoni mwa msimu uliopita, lakini taarifa kutoka ndani ya klabu zinaeleza kuwa mazungumzo baina ya uongozi wa Yanga SC na kiungo huyo raia wa Uganda yamefikia hatua nzuri, na kuna uwezekano mkubwa wa kusaini mkataba mpya wa mwaka mmoja.


Yanga SC, ambayo imeshatwaa jumla ya mataji 31 ya ligi, inatarajia kuendelea na kampeni zake za kutawala soka la Tanzania na kufanya vizuri kimataifa, na inamtazama Aucho kama sehemu muhimu ya safu ya ulinzi na uongozi ndani ya dimba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad