Milioni 900 Zampeleka Zimbwe Yanga...Asaini Miaka Miwili



Taarifa mbaya kwa mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc zinaeleza kwamba nahodha mkuu wa klabu hiyo Mohamed Hussein (Tshabalala) amefanya maamuzi magumu ya kujiunga na watani wao wa jadi yaani Yanga Sc.



Chanzo cha taarifa hii kimeeleza wazi kwamba Mohamed Hussein tayari amesaini mktaba wa miaka miwili ya kuwatumikia Yanga Sc na muda wowote kuanzia sasa atatangazwa kuwa nyota mpya wa klabu hiyo.

Taarifa za ndani kabisa zinaeleza kwamba Tshabalala amesaini Yanga Sc kwa dau la Milioni 900 za za kitanzania, hii inatajwa kuwa ni ofa kubwa sana ambayo viongozi wa klabu ya Simba Sc walishindwa kuitoa kwenda kwa nyota huyo.

Mohamed Hussein anaondoka Simba Sc mara baada ya kuwatumikia kwa miaka mingi sana lakini pia akiwa na kikosi cha wekundu wa msimbazi amepata mafanikio mengi sana pengine kuliko wachezaji wengi sana walioko kikosini hapo kwa sasa.


Mashabiki na wadau wa klabu ya Simba Sc kwa sasa watakuwa wanapitia maumivu makali sana kutokana na taarifa hii lakini uhalisia unabaki palepale kwamba mchezo wa mpira wa miguu ni biashara ya pesa na Mohamed Hussein kafuata pesa Yanga Sc kwani viongozi wa klabu hiyo kwa sasa wanawaza kukisuka kikosi hicho katika namna ambayo kitakuwa bora sana kwenye michuano ya kimataifa pamoja na michuano ya ndani.

Yanga Sc wamepata mchezo bora ambaye anaenda kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo kutokana na aina ya uzoefu aliokuwa nao kwa muda wote ambao amecheza ndani ya klabu ya Simba Sc.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad