Klabu ya Santos Sc ya Brazil imetangaza kumsajili nyota wake wa zamani, Neymar Jr kwa mkataba wa miezi 6 mpaka Juni 2025 baada ya Mbrazil kuvunja mkataba na iliyokuwa klabu yake Al Hilal ya Saudi Arabia.
Neymar (32) ambaye aliichezea Santos Sc mechi 225 na kufunga magoli 136 na ‘assists’ 64 kabla ya kutimkia Ulaya baada ya miaka 12 tangu alipojiunga na FC Barcelona mnamo Julai 2013.