Klabu ya Tanzania Prisons imesitisha mkataba wa Kocha Mkuu Mbwana Makata kutokana na mwendelezo wa matokeo yasiyoridhisha kwenye Ligi tangu alipopewa majukumu ya kuiongoza timu hiyo ya Jeshi la Magereza.
Kocha Shaban Kazumba na Shaban Mtupa ndio wataongoza jahazi la Tanzania Prisons kwa sasa wakati mipango ya kupata kocha mwingine ikiendelea.