Hii Ndio Thamani ya Viti Vilivyoharibiwa na Simba Jana, Walioharibu Wakamatwe


Hii Ndio Thamani ya Viti Vilivyoharibiwa na Simba Jana, Walioharibu Wakamatwe

Hii Ndio Thamani ya Viti Vilivyoharibiwa na Simba Jana, Walioharibu Wakamatwe

Mashabiki wa Simba jana wamevunja viti (256),kila kiti kina thamani ya $40 (tsh 92,800) ukizidisha unapata tsh 23,756,800.

Hii ni mara ya pili mashabiki baadhi wa Simba wanafanya vitendo hivi vya kijinga.

Hii inaweza kuleta shida kubwa kwa Simba ikiwemo kucheza mechi zake za CAF bila mashabiki,lakini pia klabu inakwenda kulipa 23m ambayo ingetumika kulipa mishahara na kusajili wachezaji wapya.

Ili kukomesha huu ujinga inabidi mashabiki waliofanya hicho kitendo wakamatwe na kulipishwa na siyo klabu….i think hiyo itasaidia kuondoa hizi tabia.

Hivi sasa uwanja wa Mkapa una CCTV camera 128 za kisasa zenye uwezo wa kutunza matukio kwa wiki mbili….hivyo ni rahisi ku-zoom na kuwakamata waarifu.

Hii leo shabiki akikamatwa na kuwekwa ndani kisha kulipishwa hawezi tena kuharibu kiti…..hii leo wanafanya hivi coz wanajua klabu italipa.

Hii siyo sawa watu wachache waache kuharibu mpira wetu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad