Yanga Yatangaza Kuutumia Uwanja wa KMC Complex Kama Uwanja wa Nyumbani




Klabu ya Yanga Sc imetangaza kuwa itautumia Uwanja wa KMC Complex kama Uwanja wake wa Nyumbani kwa mechi zote za Ligi Kuu ya NBC zilizosalia msimu huu wa 2024/25.

Taarifa ya leo Novemba 9, 2024 iliyotolewa na klabu hiyo imeongeza kuwa Young Africans Sc itautumia uwanja wa KMC Complex kama uwanja wake wa nyumbani pia kwenye mechi za Kombe la Shirikisho la CRDB na michezo mingine ya nyumbani ambayo kanuni itaruhusu kuutumia uwanja huo.

Haya yanajiri kufuatia vipigo viwili mfululizo kwa Yanga Sc (0-1 vs Azam Fc na 1-3 vs Tabora United) katika dimba la Azam Complex, Chamazi walilokuwa wakilitumia kama uwanja wa nyumbani kabla ya kuamua kutimkia KMC Complex, Mwenge Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad