Klabu ya Simba imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Bravos kutoka Angola, mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa katika michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Huo ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi, na sasa unawafanya Simba kuwa na alama tatu kibindoni kwenye msimamo wa kundi lao.
Pointi tatu ndio suala la msingi zaidi.