KOCHA mpya wa Yanga Sc, Sead Ramovic ambaye ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1, akiwa na TS Galaxy ya Afrika Kusini kwenye mechi 6 za ligi, hajashinda mechi hata moja, sare 2 na vipigo vinne.
Mjerumani huyo mwenye umri wa miaka 45 ameiongoza TS Galaxy kuvuna alama 2 tu huku timu hiyo ambayo ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ikifunga magoli 4 na kuruhusu 8.