Uongozi wa Simba umesikitishwa na vitendo visivyo vya kiungwana vilivyofanywa na viongozi wa Pamba FC kwa kushirikiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda kwa kutumia askari polisi mkoani humo.
Klabu ya Simba imeendelea kwa kueleza kuwa Mhe. Mtanda ni mlezi wa timu ya Pamba Jiji FC na shabiki wa wazi wazi wa timu ya Yanga.
Simba imelaani vitendo vya matumizi ya dola katika mpira wa miguu na kuwakumbusha viongozi wenye mamlaka kutumia vizuri mamlaka yao.