Kocha Gamondi Hajafukuzwa Yanga.....
Baada ya Yanga kupoteza mechi mbili mfululizo za Ligi kwa kufungwa 1-0 na Azam FC na 3-1 na Tabora United tetesi zilitamalaki kuwa Kocha wao Mkuu ambaye ni Raia wa Argentina Miguel Gamondi anakwenda kufutwa kazi lakini kwa kujitokeza kwake mazoezini leo ni dhahiri kwamba bado yupo kibaruani.
Leo Yanga SC wameendelea na mazoezi ya gym kama kawaida katika viwanja vya Gymkhana ambapo Miguel Gamond amefika kuendelea na majukumu yake ya kazi kama kawaida……. yani kwa lugha nyepesi ni kwamba Gamondi bado yupo Jangwani tofauti na uvumi uliopo mitaani kuwa amepigwa chini.