Kocha Gamondi Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Toka Ameachana na Yanga



Aliyekuwa kocha wa Klabu ya Yanga, Miguel Gamondi, ametoa ujumbe wa shukrani kwa mara ya kwanza baada ya kuondoka rasmi klabuni humo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Gamondi amewashukuru Wananchi, wachezaji, na kila mmoja aliyemsaidia katika safari yake ya kufundisha Yanga SC.

Katika ujumbe wake, Gamondi aliandika:

"Thank you very much, 🙏 Asante sana Wananchi, to my players, and everybody. I am very grateful and proud to be part of Yanga in my time. You will always be in my heart. Much love."

Maneno haya yameacha hisia tofauti kwa mashabiki wa Yanga, wengi wakimkumbuka kwa mafanikio aliyoyapata akiwa kocha wa timu hiyo.

Licha ya changamoto mbalimbali, Gamondi aliiongoza Yanga katika nyakati za ushindani mkubwa, akipigania heshima ya klabu hiyo kwenye ligi ya ndani na mashindano ya kimataifa.

Miguel Gamondi atakumbukwa kwa mbinu zake za kiufundi, utulivu wake wa kipekee, na jinsi alivyowahamasisha wachezaji wake kupigania ushindi hadi dakika ya mwisho. Kwa mashabiki wa Yanga, ataendelea kuwa sehemu muhimu ya historia ya klabu hiyo.


Kwa sasa, bado haijabainika kocha huyo ataelekea wapi, lakini ujumbe wake wa kuaga umeacha alama kubwa kwa Wananchi wa Jangwani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad