Tuchel Kocha Mpya England

 

Tuchel Kocha Mpya England

Chama cha soka Nchini England (FA) kimetangaza Thomas Tuchel kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa hilo kwa mkataba wa miezi 18 kuanzia Januari 2025 ambao utambakisha kwenye hatamu mpaka mwishoni mwa kombe la Dunia 2026.


Tuchel (51) raia wa Ujerumani anakuwa kocha wa tatu mgeni kuinoa Timu ya taifa ya England baada ya Sven Goran Eriksson raia wa Sweden na Fabio Capello raia wa Italia huku akiteuliwa kufuatia msako mkali wa makocha ambao pia ulimhusisha Pep Guardiola wa Manchester City.


Meneja huyo wa zamani wa Chelsea, Borussia Dortmund, PSG Bayern Munich anachukua mikoba ya Gareth Southgate aliyejiuzulu nafasi hiyo baada ya England kupoteza dhidi ya Uhispania kwenye fainali ya UEFA EURO 2024.


Aidha FA imethibitisha kuwa kocha wa muda Lee Carsley ataendelea kuiongoza England kwa mechi zao mbili zilizosalia za UEFA Nations League dhidi ya Ugiriki na Jamhuri ya Ireland mwezi ujao kabla ya kurejea kwenye nafasi yake kama kocha wa vijana chini ya umri wa miaka 21.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad