Simba Waichapa Prisons Uwanja wa Sokoine

Simba Waichapa Prisons Uwanja wa Sokoine

 Simba Waichapa Prisons Uwanja wa Sokoine

Timu ya Simba SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.


Bao pekee la Simba SC leo limefungwa na beki Mcameroon, Che Fondoh Malone Junior dakika ya tano tu ya mchezo akimalizia mpira uliomponyoka kipa kipa Adam Mbise kufuatia shuti la mpira wa adhabu la kiungo Kibu Denis Prosper.


Kwa ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi wanafikisha pointi 16 katika mchezo wa saba na kusogea nafasi ya pili, nyuma Singida Black Stars yenye pointi 19 baada ya wote kucheza mechi saba.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad