Timu ya wanawake Klabu Simba SC, Simba Queens imefanikiwa kushinda nafasi ya tatu baada kuichakaza bila huruma magoli manne bila majibu timu ya CEASIAA katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu wa Ngao ya Jamii kwa timu za mpira wa miguu za wanawake
Simba Queens ilitolewa na Yanga Princes hatua ya nusu fainali kwa mikwaju ya penati huku CEASIAA akitolewa na JKT Queens.
Baada ya mchezo huo, fainali inawakutanisha Yanga Princes na JKT Queens katika uwanja wa KMC jioni hii, Saa 9:30.