Simba Gari limewaka, Waitandika Namungo bao 3
Wekundu wa Msimbazi, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.
Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na beki mzawa, Shomari Salum Kapombe dakika ya nne, viungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 33 na Muangola mwneye uraia wa Kongo pia, Debora Fernandes Mavambo dakika ya 85.
Simba SC inafikisha pointi 19 baada ya ushindi huo na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi tatu na Singida Black Stars baada ya wote kucheza mechi nane.