Kocha Gamondi |
“Ninaridhishwa na kiwango cha wachezaji wangu. Inawezekana kuna nyakati mambo hayaendi sawa lakini siangalii mchezaji mmoja mmoja huwa naangalia zaidi matokeo ya timu. Mchezaji kuwa na siku mbaya kazini ni kawaida duniani kote hata kwa wachezaji wakubwa Ulaya.
“Hata hivyo naridhika na mwenendo wa wachezaji wangu wote. Mimi sina wasiwasi kabisa na timu yangu, sijui haya yanatoka wapi. Kama unajua mpira huwezi kuwa na mashaka na Yanga.”
“Nafikiri wale ambao wanajiuliza uliza maswali watapata majibu, muda utaongea” —— kocha wa Yanga Sc @miguelgamondi akizungumza kuelekea mchezo dhidi ya Pamba Jiji Fc utakaopigwa katika dimba la Azam Complex Chamazi kesho Oktoba 3, 2024.