Kocha Fadlu Alitambua Kabisa Atafungwa na Yanga
Kocha wa Simba Fadlu Davids kabla ya mchezo wa Derby ya Kariakoo alienda katika mchezo huo kwa taadhari kubwa na kabla ya mchezo huo alisema;
“Ni mechi muhimu sana kwa sababu timu zote zinaangaliwa sana, ni mechi muhimu sana kwenye ligi lakini haitaamua ubingwa wa ligi”
“Tumefuatilia mechi zao na tunawafahamu jinsi wanavyoenda kucheza mechi zao na tumefanyia kazi, kiwango na historia kwenye mechi hizi hazina nafasi sana kwa sababu kwenye derby timu itakayokua bora ndiyo itashinda mechi.”