KOCHA AS VITA AWAPA SIMBA FAILI LA MPANZU

 

KOCHA AS VITA AWAPA SIMBA FAILI LA MPANZU

Kaimu Kocha Mkuu wa AS Vita ya DR Congo, Raoul Shugu amesema Simba wamepata mtu kumsajili aliyekuwa mchezaji wa timu yake, Elie Mpanzu ambaye amejiunga na kikosi cha wekundu hao wa msimbazi kwa mkataba wa miaka miwili.


Kocha huyo amesema anafahamu uwezo wa Mpanzu kwani anaweza kucheza winga na namba 10 kulingana na matwaka ya kocha hivyo atawasaidia Simba kufikia malengo yao.


“Mchezaji mzuri kabisa ana uwezo wa kufunga mabao mengi sana na atawasaidia, usimuone umbile lake dogo suala la mpira mguuni yuko vizuri,” amesema Shungu.


Ameongeza kuwa Simba wamepata mtu wa kusaidiana na waliopo ndani ya timu hiyo na kupata kile ambacho kinatarajiwa kwa mashabiki kuona timu hiyo inapata mataji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad