Aliyekuwa kocha wa Liverpool, Jürgen Klopp ameteuliwa kuwa mkuu wa idara ya soka ndani ya kampuni ya Red Bull ambapo atakuwa na jukumu la kuratibu shughuli zote za soka katika vilabu vilivyopo chini ya Kampuni hiyo kama vile RB Leipzig ya Ujerumani na RB Salzburg ya Austria.
Klopp (57) raia wa Ujerumani atarejea rasmi katika shughuli za mpira wa miguu kuanzia Januari Mosi, 2025 ambapo pia atahusika katika mradi wa kusaka vipaji katika vilabu hivyo.
Klopp ameelezea shauku yake kwa mradi huo, akisema mapenzi yake ya soka bado hayajapungua licha ya mabadiliko katika majukumu huku akilenga kukuza na kuboresha vipaji ndani ya Kampuni hiyo.