HATIMAYE MO DEWJI ATAMBULISHA MCHORO WA UWANJA WA SIMBA

 

HATIMAYE MO DEWJI ATAMBULISHA MCHORO WA UWANJA WA SIMBA

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mo Dewji hii leo amezindua rasmi ramani ya mchoro wa kambi mpya ya Simba iliyopo Bunju jijini Dar Es Salam.

Mchoro huo unaonesha namna ambavyo Uwanja wa Mo Simba Arena utakavyokuwa baada ya kufanyiwa maboresho, ambayo kimsingi tayari yalikwisha kuanza kwa kuzungushia uzio eneo la uwanja huo.

Mo Dewji ambaye ndiye anaongoza mkutano huo wa mwaka 2024, ameweka wazi malengo na ndoto zake za baadae kwa Simba.

“Hii ni ramani mpya ya Mo Simba Arena. Mradi mkubwa ambao utaweka msingi wa mafanikio yetu baadae.

“Tunatarajia kujenga kambi bora ya mazoezi itakuwa na gym, majengo ya malazi, kituo cha lishe, bwala la kuogolea, kituo cha burudani, viwanja vitano vya kisasa zaidi ya hayo kujenga makumbusho ya klabu na kuanzisha chuo cha maendeleo ya vijana ili kulea vipaji vya soka nchini.” Amesema Mo Dewji

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad