Elia Mpanzu |
Klabu ya Simba SC imemtangaza rasmi Mpanzu Elie Nkibisawala, raia wa Congo mwenye umri wa miaka 22, kuwa mchezaji wao atakayeitumikia timu hiyo msimu wa 2024/2025 hadi 2025/26
ANAITWA : ELIE MPANZU KIBISAWALA
UMRI : 22
URAIA : CONGO
NAFASI : WINGA /KIUNGO MSHAMBULIAJI
SIFA : KASI ,KUPIGA CHENGA NA KUTUMIA MIGUU YOTE MIWILI
Elie mMpanzu alikuwa ndo mchezaji muhimu zaidi as vita 👇
Msimu uliopita AS VITA CLUB walifunga jumla ya magoli 36 huku elie mpanzu akifunga magoli 10 na asist 12 yani jumla alihusika kwenye goli 22 yani karibu asilimia 60+
MUHIMU : dirisha la usajili CAF linafungwa leo saa 5:59 na tayari jina la elie mpanzu tayari lishaingizwa kwenye system na ataanza kutumika kwenye hatua ya makundi huku akisubiri dirisha la ndani aingizwe kwenye system atumike pia kwenye ligi na baada ya kutambulishwa tu elie mpanzu ataanza rasmi kujifua na SIMBA kwani tayari keshakabidhiwa vifaa vyake vya mazoezi na atahusika na program zote chini ya mwalimu fadlu davies
HII NI MALI HALALI YA SIMBA