AZAM TV 'MAMBO SAFI' MECHI ZA CAF MSIMU HUU, ATANGAZWA KAMA MSHIRIKA

 

AZAM TV 'MAMBO SAFI' MECHI ZA CAF MSIMU HUU, ATANGAZWA KAMA MSHIRIKA
Azam TV vs CAF

Shirikisho la Soka barani Afrika, (CAF), limeitangaza rasmi Azam TV kuwa mshirika wake kwenye mashindano yake makuu msimu huu wa 2024/25.


Mashindano hayo ni pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF CL), Kombe la shirikisho Afrika (CAF CC), Ligi ya Mabingwa Afrika kwa wanawake (CAFWCL) pamoja na CAF Super Cup (CAF SC)


Hii maana yake ni kwamba, mashindano yote makubwa ya CAF ngazi ya vilabu msimu huu utaendelea kuyapata kupitia chaneli za michezo za Azam TV, yaani Azam Sports 1 HD, Azam Sports 2 HD,Azam Sports 3 HD na #Azam Sports 4 HD


Kazi yako ni kulipia tu kisimbuzi chako kwa wakati…..


Kumbuka droo ya kupanga makundi ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho itafanyika Oktoba 7 na itakufikia mbashara kupitia Azam TV

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad