Beki wa kushoto wa Simba SC, Mohammed Hussein (Zimbwe) amesema haumizwi na wanaomfananisha kwa ubora na wachezaji wengine wanaocheza nafasi yake kwa bali wanampa nguvu ya kuongeza juhudi na ubora wake ndiyo maana ashuki kiwango.
Zimbwe amesema hawezi kuzuia watu kumfananisha na wengine kwa ubora wala haumizwi na wanaombeza kwa kumwita mzee kwa sababu hana uzee wowote ndiyo maana anaendelea kukipiga katika kikosi cha kwanza Simba.
“Mi huwa sichikizwi na wanaonibeza wala kunifananisha na wachezaji wengine kwa bali wananitia nguvu zaidia ya kupambana na kuonyesha uwezo wangu ndiyo maana hadi leo naendelea kucheza vizuri,
“Mi nina uzee gani? Siwezi kuwakataza watu wasiniseme kwa sababu wana uhuru wao lakini maneno kwangu ndiyo yananipa nguvu ya kufanya vizuri zaidi katika uchezaji wangu,” alisema Zimbwe.
Zimbwe pia alisema huwa hapati majeraha ya mara kwa mara kwa sababu huwa anajilinda sana kwa mazoezi na kimwili.
Beki huyo amesema kuumia kwa mchezaji ni sehemu ya mchezo lakini pia hutokea kwa mapenzi ya Mungu hivyo yeye anajitahidi kujilinda lakini pia humuomba Mungu wake ili asipate majeraha ya mara kwa mara.
“Mimi sipati majeraha ya mara kwa mara kwa sababu najilinda sana lakini pia ni Mungu tu huwa namuomba nisipate majeraha ya mara kwa mara,” alisema.